Naibu Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshugulikia Kazi, Ajira na
Vijana ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma Mjini Anthony Mavunde ametimiza
ahadi ya kumkabidhi katika shule ya Fountain Gate Academy mtoto
Christopher Elias ambaye alikatwa miguu yote katika hospitali ya
Benjamin Mkapa iliyopo Dodoma baada ya kupatikana na maradhi ambayo
hayakubainishwa kwa sababu za kitaalam.